Mwanamuziki wa nchini Rwanda mwenye nyota na kipaji cha kipekee cha
muziki, Mani Martin ataiwakilisha nchi yake Rwanda kwa kushiriki katika
tamasha la kimataifa la muziki called Bayimba huko Uganda.
Tamasha hili ambalo safari hii linafanyika kwa mara ya 6,
linatarajiwa kuanza mwezi ujao huko Jinja, na ni nafasi nzuri kwa
wasanii wakongwe pamoja na wale wanaochipukia kuonyesha vipaji vyao kwa
wapenzi wa
sanaa hiyo.
sanaa hiyo.
Mani ambaye mbali na muziki pia ni mtunzi mzuri wa mashahiri pamoja
na mwigizaji, ameendelea kujijengea jina kubwa katika majukwaa ya
kimataifa hasa kutokana na muziki wake wenye vionjo vya kiafrika na
ladha za kiasili ambao dunia imeupokea vizuri


