Jaguar kutoka Uhuru Land, Kenya ambaye kwa sasa chupa lake la Kipepeo
ambalo ndio linasubiriwa kwa hamu kitaa, amegusa mioyo ya wengi baada ya
kujitolea kumsomesha mwanafunzi David Owira ambaye ni msanii
anayetokea katika mazingira magumu.
David alikuwa anahitaji kiasi cha shilingi za kikenya 200,000 zaidi
ya shilingi milioni 3 na laki 8 za kibongo, ada ya kidato cha pili mpaka
cha nne, pesa ambayo Jaguar amejitolea kusafisha yote.
Jaguar kwa sasa nyota yake imeonekana kung’ara kipesa kutokana na
dili kibao ambazo amekuwa akizipiga hadi kufikia hatua ya kununua ndege
yake binafsi ukiachia mbali magari ya kifahari ambayo anamiliki


0 comments:
Post a Comment